Mpasua Msonobari  -  Ushindi wa Simba wamkubusha Mo Dewji, alivyokuwa mbunge Singida Mjini

Mpasua Msonobari - Ushindi wa Simba wamkubusha Mo Dewji, alivyokuwa mbunge Singida Mjini

Mpasua Msonobari

5 лет назад

589 Просмотров

Magoli 2 Yaliyoipatia ushindi Simba SC ya Tanzania almaarufu "Wekundu Wa Msimbazi" dhidi ya timu ya AS Vita ya DRC Congo almaarufu "Black Dolphins" Yani Pomboo Weusi.
Ushindi wa Simba wamkubusha Mo Dewji, enzi zile akiwa mbunge Singida Mjini

[Rais Magufuli leo katika habari leo wameangaziwa pamoja na Makonda na Pierre Liquid/ Konki Liquid katika Azam TV wakikashifu masuala ya ngono.]

Jumamosi asubuhi ilikuwa asubuhi ya kawaida tu kwa Daron Mo, shabiki sugu wa Simba SC inayomilikiwa na Mohamed Dewji, mjasiriamali kindakindaki wa kiafrika, mmiliki na Rais wa MeTL Group, mwasisi wa wakfu wa Dewji na aliyewahi kuwa mwanasiasa maarufu, mbunge wa Singida mjini!

Hata hivyo, Jumamosi jioni Daron Mo alipokuwa kwenye foleni ya kuingia katika Uwanja Wa Taifa Dar Es Salaam, hali haikuwa ya kawaida kamwe! Alijawa na furaha furifuri na tumaini kubwa kwamba Wekundu wa Msimbazi hawatambwaga.

Daron Mo alipoyaangaza macho yake, mashabiki walikuwa wameujaza uwanja mzima wa Taifa na ukajaa furifuri, hadi kuwatema mashabiki wengine ambao iliaminika kwa ujumla pamoja na wa uwanjani walikuwa takribani 60,000. Makamanda, wachezaji wa Simba SC walikuwa wamewasili uwanjani kwa madaha na mikogo, kule faraghani walikuwa wakijiandaa, wakawa wanatiana shime na motisha kwa namna yao wenyewe. Kufumba na kufumbua, kikosi hicho kilijitoma uwanjani na mechi ikang'oa nanga, huku wingu angani likiwa angavu na mpwitompwito wa mashabiki ukishinikiza uwanjani. Simba SC Sifuri nayo AS Vita Sifuri.
............................................................................................
Mwalimu wa klabu ya Simba SC, Patrick Aussems alikuwa na haya ya kusema baada ya mechi kukamilika, namnukuu: "Tunaiandika historia ya Simba ... Twawashukuru wachezaji, wafanyikazi wangu naye Mo! Asanteni sana mashabiki kwa kuyawezesha na kuyasababisha mazingira haya ya ajabu! Tumeingia kwenye robo fainali, hebu na sasa tufikeni kwenye nusu fainali ..."

Daron Mo alipokuwa akizivua nguo zake chumbani akienda zake kulala Jumamosi usiku wa manane, baada ya kutoka kwenye uwanja wa taifa kuitazama mechi hiyo ya kihistoria, hakuwa bado anaamini kuwa Simba SC nayo kawavaa AS Vita. Naam, kazi yao uwanjani ilikuwa moja tu, kuupata ushindi, na ushindi walikuwa wameupata!

Mimi ni Mpasua Msonobari, nikiripotia Sasafrica Productions, Zanzibar Visiwani.

Usikose kujiunga yani kusubscribe katika Youtube channel yangu - @Msonobari.

Mpasua Msonobari is available on:
YouTube: https://www.youtube.com/user/msonobari/

Facebook: https://www.facebook.com/msonobari/

Instagram: https://www.instagram.com/mpasuamsonobari/

Twitter: https://twitter.com/msonobari/

SoundCloud: https://soundcloud.com/msonobari

SoundBetter: https://soundbetter.com/profiles/129686-mpasua-msonobari

For Bookings & Correspondence:
Call: +254 725 084 032
Email: [email protected]
Zanzibar, Visiwani

#MpasuaMsonobari #CAFCL, #ThisIsSIMBA, #Modewji #HashtagMpasuaMsonobari #Tanzania #ChurchillShow

Тэги:

#10NTrending #SimbaSC #ASVita #SimbaYashinda #MagoliYoteYaSimba #MeTL_Group #SimbaSCTanzania #DewjiFoundation #WEF #PatrickAussems #Georgetown #CAFCL #ThisIsSIMBA #NguvuMoja #YGL #Hoya #DreamBigger #TukutaneTaifa #DoOrDie #Bwakila #ShabbyDenco #simba_2019
Ссылки и html тэги не поддерживаются


Комментарии:

@josephgomalo41
@josephgomalo41 - 20.03.2019 23:11

wewe Msonobari Mpasuaji ndio mtangazaji makini sana.. yaani raha mpaka lahaaa..! keep it up brother..!

Ответить
@rosaleon1836
@rosaleon1836 - 25.07.2019 07:47

Simba hadi mwisho.

Ответить